Bwawa la kuogelea lililopo katika Hoteli ya Itungi Lodge kata ya Vingunguti jijini Dar es salaam
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ,Omary Kumbilamoto kabla ya kuzindua bwawa la kuogelea na hoteli hiyo ya Itungi Lodge katika kata ya Vingunguti jijini Dar es salaam. 
Naibu Meya wa Manispa ya ilala akiwa ameongozana na wajumbe wanzake kukagua sehemu ya bwawa la kuogelea lililopo katika Hoteli ya Itungi kata ya Vingunguti 
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala akikata utepe kuashiria uzinduzi wa bwawa la kuogelea na hoteli ya kitalii ya kwanza kujengwa Vingunguti 
Mkurugenzi wa Hoteli ya Itungi Lodg,Nicholas Andrew Mwituka akizungumza katika hafla hiyo.



Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe Omary Kumbilamoto amezindua hoteli mpya ya kitalii na bwawa la kwanza la kuogelea katika kata ya Vingunguti jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.

Akizungumza na wakazi wa Vingunguti wakati wa uzinduzi wa Hoteli hiyo ya Itungi Lodge, Kumbilamoto amesema kuwa bwawa hilo ni moja ya vivutio vipya vya Vingunguti kwani ndio la kwanza tangu kuanza kuundwa kwa mji huo ambao ni maarufu kwa machinjio ya Nyama.

“Mtu unaweza kuona kama ni kitu cha kawaida lakini ni jambo kubwa sana kwani kuanzia Kariakoo mpaka unafika Gongolamboto bwawa la kuogelea ni moja tu kwa sasa ambalo linapatikana hapa Vingunguti hivyo tunapaswa kujivuna na kumsifu muwekezaji huyu” amesema Mhe. Kumbilamoto. 

Kwa upande wake Mkurugenzi na mmiliki wa hoteli hiyo Bw. Nicholas Andrew Mwituka amewaomba wakazi wa Vingunguti kutumia uwepo wa hoteli hiyo kama fursa ya kujiongezea kipato na ajira mpya kwa vijana wanaozunguka eneo hilo.

Amesema kuwa wageni wote kutoka nje ya nchi ambao watakuja kununua nyumba hapo Vingunguti hawatakuwa na sababu ya kwenda kulala mbali hivyo pesa zote na huduma za kisasa watazipata hapo hapo Vingunguti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...