
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, akikata utepe kuzindua mafao ya Fidia na na ubia baina ya watoa huduma za afya .Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mhagama kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam, Desemba 20, 2016. wanaoshuhudia ni Naibu Mawaziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Mh. Anthony Mavunde, (wapili kulia), Mh. Dkt. Abdallah Possi, (watatu kulia), Bw. Emmanuel Humba, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), wanne kulia, na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba. (watano kulia). .( PICHA NA MUHIDIN SUFIANI)
NA ANTHONY JOHN, GLOBU YA JAMII
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge kazi ,vijana Ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Muhagama, amewataka waajili wote kuwasilisha Michango ya wafanyakazi wao Mfuko Fidia kwa Wafanyakazi WCF kwa wakati.
kwa Mwaka huu wafedha Serikali imewasilisha Michango ya wafanyakazi wake wote ambapo alizitaka Sekta binafsi pia kuwasilisha Michango yao kwa wakati.Sanjari na Hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Masha Mshomba ameongeza kuwa Mpaka kufikia Novemba 30 Mwaka huu Jumla ya waajili 5945 wamechangia na wamepewa na ya usajili.Akizungumza katika Uzinduzi wa Huduma za utoaji wa Mafao ya fidia kwa wafanyakazi na ubia kati ya Mfuko na watoa Huduma za Afya amesema kuwa
Hata Hivyo Mweketi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko huo Emmanuel Humba amesema Mfuko Huo utachangia kwa kiwango kikubwa Sera ya Tanzania ya Viwanda iliyoa anzishwa na Serikali ya awamu ya tano kwani wafanyakazi watakapo kuwa na Afya njema watafanya kazi kwakujiamini na kuleta Maendeleo.

Waziri Mhagama, akimkabidhi cheti cha ubia baina ya WCF na watoa huduma za afya, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bernard Konga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji wa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi na Ubia kati ya Mfuko na watoa huduma za afya, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.
Waziri Mhagama, akimkabidhi cheti cha ubia baina ya WCF na watoa huduma za afya, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Mkifupa (MOI), Dkt. Othman Kiloloma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji wa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi na Ubia kati ya Mfuko na watoa huduma za afya, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...