Na John Gagarini

TAASISI ya Misaada ya Bo’s Love Childrens Home Foundation kutoka nchi ya China imetoa msaada wa kiasi cha shilingi milioni 25.2 na vyakula kwenye kituo cha kulea watoto cha Msimbazi kilichopo Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Christmass na kuukaribisha mwaka mpya wa 2017.

Akizungumza na waandishi baada ya kukabidhi fedha na vyakula hivyo kwenye kituo hicho ikiwa ni sherehe ya uzinduzi wa taasisi hiyo mwenyekiti wa shirika hilo Bo Sun alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo kwa ajili ya kuwafariji watoto wasiokuwa na wazazi wanaoishi kwenye kituo hicho.
Sun alisema kuwa walitembelea na kuona jinsi gani watoto hao wanavyolelewa kwenye kituo hicho na kuona kuwa kituo hicho kinahitaji misaada ya hali na mali kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao.

“Tumekuwa tukisaidia vituo mbalimbali vya kulea watoto na yatima na watu wanaotusaidia wamekuwa wakichanga fedha kwa ajili ya kuwasaidia ili nao wapate faraja,” alisema Sun.Aidha alisema kuwa fedha zilizotolewa ni michango ya wafanyabiashara mbalimbali wa China ambao wako hapa nchini na wameguswa na jambo hilo na kuamua kusaidia kituo hicho.

“Kuna wawakilishi watendelea kukisaidia kituo hichi na hata maeneo mengine kwa watoto wenye mahitaji tunaomba na watu wengine wajitokeze kusaidia watoto kama hawa kwani wanahitaji upendo,” alisema Sun.

Akishukuru kupatiwa misaada hiyo ya chakula na fedha taslimu mkuu wa kituo hicho cha kulea watoto Anna Francis alisema kuwa kituo chake kinashukuru kwa msaada huo na kuwataka watu zaidi wajitokeze kusaidia.
Francis alisema kuwa changamoto kubwa waliyonayo ni fedha kwa ajaili ya kuwalipa mishahara watumishi 24 ambao wanawahudumia watoto waliopo kwenye kituo chake.

“Tuna watoto 52 na tunawashukuru watu kama hawa wanaokuja kutusaidia lakini mbali ya changamoto ya fedha pia magonjwa nayo ni changamoto kubwa sana ambapo watoto wamekuwa wakiugua mara kwa mara,” alisema Francis.
 Mkuu wa kituo cha kulea watoto cha Msimbazi Sista Anna Francis akiwa amebeba mtoto akiwa na wageni waliotembelea kituo hicho na kutoa misaada ya vyakula na fedha.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Bo’s Bo Sun aliyemshika  mtoto wa kituo cha kulea watoto cha Msimbazi akiwa na baadhi ya wageni waliojitolea michango kwa ajili ya kukisaidia kituo hicho wakiwa katika picha ya pamoja
 Bo Sun mwenyekiti wa taasisi ya Bo’s katikati ba Sara Hong wakikabidhi fedha kwa mkuu wa kituo cha kulea watoto cha Msimbazi Anna Francis walipotembelea kituo hicho kutoa misaada ikiwemo ya chakula na fedha.
Baadhi ya watoto wakiwa na walezi wao kwenye kituo hicho cha kulea watoto cha Msimbazi.   

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...