Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Wakazi zaidi ya 200 wa kata ya buguruni waridhia kumpisha muwekezaji kujenga Kiwanda kikubwa  ili kutekeleza sera ya Viwanda nchini.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto amesema kuwa wakazi hao ambao mara ya kwanza waligoma kwa hofu ya fidia wameamua kuridhia mradi huo baada ya kikao cha mkuu wa mkoa na Muwekazaji huyo.

“Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikaa na muwekezaji na kukubali kulipa fedha ambayo wananchi hawa wataridhika nayo hivyo ameniagiza mimi nije niunde kamati ya watu tisa ambao watawakilisha wengine katika kikao kimoja kitakacho kutanisha mkuu wa mkoa na muwekzaji huyo”amesema Kumbilamoto.

Ameongeza kuwa katika kundi hilo la watu tisa kutakuwa mwenyekiti, katibu ,katibu msaidizi na wajumbe wengine kutoka kundi hilo la watu hao.

Ametaja kuwa katika kutekeleza sera ya Rais John Pombe magufuli kwenda katika Tanzania ya Viwanda ni vyema kukawa na maridhiano mazuri baina ya muwekezaji na wananchi ili kupunguza migogoro isiyokuwa ya lazima.

Ametaja kuwa pindi zoezi hilo la ulipaji wa fidia litakapo kamilika eneo hilo litaweza kujengwa kiwanda kikubwa kitakachoweza kuajiri watu zaidi ya 1000.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala akizungumza na wakazi wa Kata ya vingunguti katika kikao cha maridhiano juu ya muwekezaji kununu nyumba zao.
Wakazi wa Vingunguti wakimsikiliza kwa Makini Naibu Meya Omary Kumbilamoto juu ya mpango wa muwekezaji huyo na maagizo kutioka kwa mkuu wa mkoa.
Naibu meya Omary Kumbilamoto akiteta jambo na baadhi ya wakazi wa eneo hilo katika eneo ambalo nyumba zinahitaji kununuliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...