MAREHEMU DEUSDEDITI M. GOGADI.
Ni siku, miezi hatimaye mwaka mmoja sasa tangu ulipotangulia mbele za haki mpendwa baba yetu DEUSDEDITI M. GOGADI.
Hatutasahau upendo, ucheshi na busara zako daima pengo lako halitazibika kamwe. Unakumbukwa sana na mke wako Tecla Gogadi, watoto wako Jacqueline, Neema na Monica Gogadi, mkwe wako, mashemeji zako, ndugu, jamaa na marafiki.
Mkesha wa kumuombea baba yetu utafanyika Nyumbani Kijitonyama tarehe 30/12/2016 kuanzia saa mbili na asubuhi tarehe 31/12/2016 saa 12.30 asubui tutajumuika katika ibada Takatifu Kanisa Katoliki la Mwenge Maximilian Kolbe jijini Dar es salaam.
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA NURU YA DAIMA IMWANGAZIE APUMZIKE KWA AMANI. AMEEN.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...