Na Jacquiline Mrisho –
MAELEZO
Utafiti wa Viashiria
vya Virusi vya UKIMWI (VVU) na Maralia (THMIS) wa mwaka 2011/2012 kwa upande wa
Tanzania Bara vinaonyesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wameambukizwa ugonjwa
huo kuliko wanaume.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Jenista Mhagama alisema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa asilimia
6.2 ya wanawake wameambukizwa ugonjwa wa ukimwi ikilinganisha na asilimia 3.8
ya wanaume.
Waziri Mhagama alisema
kuwa kutokana na utafiti huo, maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa upande wa
Tanzania Bara ni asilimia 5.3 na inakadiriwa
kuwa jumla ya watanzania
1,538,382 wanaishi na VVU ambapo vijana wenye umri kati ya 15-24 ni asilimia
10.6 na watoto walio chini ya miaka 15 ni 11.8.
“UKIMWI bado ni janga
kubwa nchini Tanzania kwani takwimu zinaonyesha kuwa maambukizo mapya yanakadiriwa kufikia watu 48,000
kwa mwaka hali ambayo inaashiria kupoteza nguvu kazi kubwa katika nchi yetu”
Kwa mujibu wa Waziri
Mhagama alisema Tanzania itendelea kushirikiana na nchi nyingine Duniani kuhakikisha
wanatokomeza janga la ugonjwa huo ifikapo
mwaka 2030.
Aliongeza kuwa
Serikali inaendelea kuwahamisha wananchi waendelee kujitokeza kupima afya zao
ili wajitambue na kujua namna ya kujilinda kwani Shirika la Afya Duniani (WHO)
linasisitiza nchi wanachama kuwaanzishia dawa mara moja watu wote watakaopima
na kugundulika kuwa na VVU.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dr. Leonard Maboko alisema
kuwa kwa mwaka 2015 walioambukizwa VVU walikuwa Watanzania 2,100,000 ambayo ni
idadi kubwa ukilinganisha na idadi ya sasa lakini pamoja na kushuka kwa idadi hiyo wananchi
wanatakiwa kuendelea kujilinda mara dufu.
”Ingawa maambukizi ya
VVU yameshuka kutoka Watanzania 2,100,000 hadi 1,538,382, Watanzania hatutakiwi
kubweteka bali tunatakiwa tufanye jitihada za pamoja kuhakikisha janga hili
linafikia mwisho,”alisema Dr. Maboko.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu siku ya UKIMWI Duniani, kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dr. Hamis Mwinyimvua.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dr. Leonard Maboko akifafanua juu ya takwimu za maambukizi ya UKIMWI wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...