Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Hali ya biashara imeonekana kuwa na mwenendo wa kawaida katika machinjio ya vingunguti kutokana na kutokuwepo kwa bei za kilanguzi hasa kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya.

Globu ya jamii imetembelea katika machinjio hayo na kujionea namna biashara zinavyofanyika, huku baadhi ya wauza nyama wakieleza kuwa hali imekuwa ya tofauti na miaka ya nyuma,kwani kipindi kama hiki biashara ilikuwa vizuri kwa bei za nyama kupanda maradufu mpaka shilingi elfu 12 kwa kilo.

Kwa uapande wake mchuuzi wa nyama katika machinjio hayo, Jacob Urasa amesema kuwa kwa miaka ya nyuma watu walikuwa na tabia ya kufungia mifugo na kushindwa kuileta mnadani, hali iliyokuwa ikisababisha nyama kupanda bei machinjioni kutokana na kuadimika kwa ng'ombe, lakini mwaka huu ni tofauti sana kutokana na kuwepo kwa nyama ya kutosha ambayo inapatikana kwa bei nafuu.

"Hapo zamani siku kama ya leo nyama machinjioni ilikuwa ikiuzwa kwa bei ya shilingi 6000 mpaka 7000 lakini leo ni tofauti sana kwani kwa bei ya alfajiri ni shilingi 5000 wakati kukishapambazuka  majira ya saa moja asubuhi bei inakuwa shilingi elfu 4000 kwa kilogramu moja" amesema Urasa.

Ameongeza kuwa mbali na bei hiyo lakini bado hali ya soko imekuwa ngumu kutokana na kuwepo kwa nyama nyingi na soko kuwa chache katika kipindi hiki hali ambayo ni tofauti na miaka iliyopita.

Ametoa wito kwa serikali kuendelea kusimamia vizuri machinjio hayo ambayo kwa sasa yamekuwa ni kimbilio kubwa kwa wafanyabiashara wa nyama wa mkoa wa Dar es Salaam na maeneo jirani kutokana na ubora wake .
Wauza nyama wa Machinjio ya vingunguti wakipima nyama katika mzani kabla ya kuuzwa kwa wafanyabiashara
Wauza utumbo wakikata kata kwa ajili ya kupeleka sokoni kutokea machinjio ya vingunguti, Jijini Dar.
Sehemu ya mbuzi waliopo katika eneo la njemla machinjio ya vingunguti kusubiri kununuliwa na watu kwa ajili ya kioweo cha sikukuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...