WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Stadi, Profesa Joyce Ndalichako ameitunuku nishani ya uzalendo kampuni ya Global Education Link (GEL) kutokana na mchango inaotoa katika maendeleo ya elimu nchini.

Nishani hiyo aliitoa leo wakati akizindua mkutano mkuu wa 11 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari nchini (TAHOSSA) mkoani Dodoma. 
Mkurugenzi wa Global Education Link (kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na ufundi Stadi Prof. Joyce Ndalichako.

Rais wa Wakuu wa Sekondari Tanzania (TAHOSSA), Bonus Ndimbo alisema GEL imekuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo katika elimu, sio tu kwa TAHOSSA hata kwa nchi kwa ujumla.

“Tunaipongeza sana Global Education Link, kwani imekuwa karibu na jamii, imekuwa karibu na sekta ya Elimu na maendeleo ya nchi kwa ujumla,” alisema Katibu Mkuu wa TAHOSSA Diana Matemu.Global Education Link ni kampuni iliyoanzishwa Mwaka 2006 kwa lengo la kuwaunganisha wanafunzi wa Tanzania wanaotaka kusoma vyuo vikuu vya nje.

Tangu imeanza shughuli zake kwa miaka 10 sasa, zaidi ya wanafunzi 5400 wamefaidika kwa kuunganishwa na vyuo mbalimbali vilivyoko Marekani, Canada, Uingereza, Afrika Kusini, Ukraine, India, Urusi, Malaysia, China na nyinginezo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akizungumza na Wakuu wa Sekondari Tanzania baada ya kupewa nafasi ya kipekee ya kuwawakilisha wadau mbalimbali wa elimu waliokaribishwa katika mkutano huo mbele ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Ufundi stadi Prof Joyce Ndalichako.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel (hayuko pichani).

Akizungumza baada ya kukabidhiwa nishani hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel alishukuru na kusema anafanya hivyo kwa lengo la kusaidia Serikali na Watanzania kwa ujumla katika kuharakisha maendeleo nchini.

Kikubwa ambacho Mkurugenzi wa GEL alisema ni kuwa mpango wa mafunzo kwa wanafunzi utasaidia kuwafanya wanafunzi kuchagua kozi ambazo zitakuwa na tija kwao na taifa kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...