Kikosi cha Yanga

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Ligi kuu ya Vodacom kuendelea tena kesho katika viwanja viwili kwa kwuakutanisha Mabingwa watetezi Yanga wakikutana na Ndanda kwenye uwanja wa Taifa huku Mtibwa wakiwakaribisha Majimaji uwanja wa Manungu mjini Morogoro.

Yanga wanashuka dimbani wakikumbuka sare 1-1 dhid ya African Lyon waliyoipata mwishoni mwa wiki huku Mtibwa akiondoka na ushindi wa goli 2-0 waliopata kwa Ndanda na Majimaji wakiambulia sare na Azam.

Kocha mkuu wa Yanga, George Lwamdamina ameendelea na mazoezi na kikosi chake huku Donald Ngoma akijumuika na wenzake baada ya kuukosa mchezo uliopita akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Katika mazoezi hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, wachezaji wa Yanga wameonekana kujinoa vilivyo kwani wanataka ushindi kwa hali yoyote na kuweza kuwafunga Ndanda ambapo kwenye mechi ya awali walitoka sare Mkoani Mtwara.

Ila leo kikosi cha Yanga kikiwa katikati ya mazoezi, timu ya Ndanda walifika na wao kutaka kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru na kupelekea Lwandamina kusitisha mazoezi hayo na kuwaruhusu wachezaji kwenda kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa kesho.

Mtibwa nao wamejizatiti kushinda mchezo baada ya kutoka na ushindi ugenini dhidi ya Ndanda na wamesema kuwa raundi hii ya pili itakuwa ni ya ushindi tu kwao hawatakubali kupoteza hata mchezo mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...