Kiungo wa zamani wa Manchester City, Real Madrid, Tottenham Hotspur, Arsenal , Crystal Palace na Monaco ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Togo, Emmanuel Adebayor anatajwa kuwa muda wowote kuanzia sasa ataweza kujiunga na klabu ya Yanga ya Tanzania kwa mkataba mnono.
Taarifa zilizotufikia katika globu ya jamii zinamtaja nahodha huyo wa timu ya Togo kuwa atajiunga na timu hiyo ili waweze kutetea ubingwa na kujianda na michuano ya kimataifa ya klabu bingwa Afrika.

Adebayor anataka kujiunga na wanajangwani hao ikiwa ni siku chache baada ya timu yao ya Taifa ya Togo kutolewa katika michuano ya AFCON.

Adebayor kama atajiunga na klabu hiyo ya Yanga atakuwa mchezaji wa kwanza kutoka ligi ya mabingwa ulaya kuja kucheza katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Huu sasa wehu! ivi aache kwenda kumalizia soka lake China au Marekani ambapo wengi hutamani kwa kuvutiwa na dau kubwa aje hapo? kwa dau gani hasa kwa hizi hela ambazo huitwa za madafu? Adebayor hajachoka kiasi hiko cha kutotakiwa na club hata zilizopo Uarabuni. Hii itakua ndoto vinginevyo nitaamini kwamba amerogwa kama ambavyo ilivyosemakana wakati fulani.

    ReplyDelete
  2. Habari hii imenifanya niangalie KALENDA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...