Globu ya Jamii
Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul a.k.a ‘Diamond
Platnumz’ anatarajia kuachia video ya wimbo wake mpya uitwao Rockonolo wakati
wowote kuanzia sasa, kwa mujibu wa Meneja wa Mwanamuziki huyo Jorge Mendez
ambaye ameandika katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter na kuweka
kipande cha Video hiyo na kusema inakuja hivi karibuni.
Video ya wimbo huo ambao inamuonesha mwanamuziki wa kimataifa
kutoka nchini Congo Muhombi ambaye amefanya vizuri sana kutokana wimbo huo
kutajwa kuwa ni remix ya moja ya nyimbo zake.
Mara baada ya kuweka video hiyo katika mtandao huo Mendez amepokelewa
kwa shangwe na wapenzi wa mwanamuziki huyo. Video ya Diamond na Mohombipamoja katika uzinduzi wa AFCON 2017.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...