Na Humphrey Shao,
Globu ya Jamii
Globu ya Jamii
Mkurugenzi wa kampuni ya ASETt Entertiment inayomiliki bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka, amekuja juu mara baada ya kusikia habari kuwa mwanamuziki kinara wa bendi hiyo Ali Choki anataka kuondoka.
Asha Baraka ambaye amempigia simu ripota wa Globu ya Jamii mara baada ya kuandikwa habari hizo na kusema:
“Nasema hivi... (Ali) Choki hawezi kuondoka Twanga Pepeta kwa kuwa alisaini mwenyewe mkataba wa miaka mitatu na mkataba huo unamalizika mwaka 2018. Sasa huyo anayemtaka Choki asubiri wakati ufike ndio aanze kumshawishi...” amesema Asha Baraka.
Hata hivyo Asha Baraka marufu kama "Iron Lady" (mama wa chuma) alipoulizwa juu ya mtu anayehitaji kuvunja mkataba anatakiwa kulipa kiasi gani cha fedha, amesema: "Mimi nipo na mwanamuziki kwa mkataba wa miaka mitatu. Sasa huyo anayetaka kuvunja mkataba wangu na Choki mwambie siko tayari kuzungumzia swala la kuvunja mkataba. Kwa sasa mimi nipo kwa ajili ya kuimarisha bendi na sio kubomoa bendi..."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...