Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KLABU ya Yanga imeonesha nia ya kumrudisha aliyewahi  kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Charles Boniface Mkwasa (pichani) kwenye klabu hiyo kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi la timu hiyo.
Habari za ndani ya Yanga zinasema kuwa Mkwasa atakuja kuongeza nguvu kwa timu yao kwani kwa sasa wanahitaji mtu mwenye uelewa mkubwa wa soka la Tanzania na kuonesha lengo la kumchukua baada ya kumaliza kandarasi yake na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).
Mkwasa anasadikiwa kupewa cheo kikubwa zaidi kitakachokuwa kinampa nafasi ya kusimamia timu zote ikiwemo za vijana na kutafuta vipaji nchi nzima na kuvikuza.
Taarifa rasmi ya kuja kwa Mkwasa inaweza ikatolewa hivi karibuni huku uwepo wa Juma Mwambusi kwenye benchi la wanajangwani hilo likiwa halijaweka wazi kama wataendelea nae au la.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...