Na Othman Khamis Ame, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema miradi ya Kijamii inayoendeshwa kupitia Mfuko wa wa Maendeleo ya Jamii Tanaznia {TASAF } inalazimika kuibiliwa na wananchi wenyewe katika maeneo yao kwa vile wao ndio wanaoelewa mazingira yanayowazunguuka. 
Amesema Serikali Kuu kazi yake kubwa ni kuongeza nguvu za uwezeshaji katika kuona miradi hiyo inaimarika na kukua kwa lengo la kuwaondoshea ukali wa maisha Wananchi wake katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba. 
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo akiwa katika ziara ya siku Tatu Kisiwani Pemba kuangalia miradi ya Maendeleo wakati alipokagua miradi ya Tasaf katika Bonde la Kidau Ndagoni kuona maendeleo ya ujenzi wa Tuta la kuzuia maji ya Bahari yanayoathiri wakulima wa bonde hilo. 
Alisema yapo maendeleo makubwa yaliyopatikana tokea kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF)  hasa katika kuzisaidia Kaya Maskini zilizozongwa na ukali wa maisha ziwe na miundombinu ya kujiendesha Kimaisha kupitia miradi wanayoianzisha. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi na wakulima hao wa Bonde la Kidau pamoja na wale wote wanaopata huduma kupitia mfuko wa Tasaf kutokana na juhudi kubwa wanazozichukuwa katika kuimarisha miradi yao ikiwemo ile ya sekta ya kilimo iliyokuwa tegemeo kubwa la wananchi wa Zanzibar kwa zaidi ya asilimia 8%. 
 Mhandisi wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Pemba Nd.Talib Bakari kushoto akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuangalia Tuta la kuzuia Maji ya Bahari linaloendelea kujengwa kwenye Bonde la Kidau Ndagoni kupitia Mradi wa TASAF.
 Muonekano wa Tuta la Kuzuia maji ya Bahari kwenye Bonde la Kidau Ndagoni likiwa katika hatua za mwisho kukamilika ujenzi wake kwa zaidi ya asilimia 90%. 

Balozi Seif akiangalia eneo la Bonde la Kidau ambalo limeathirika kwa maji ya Mvua akiambatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi Kulia yake.
Picha na  OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...