BMGHabari
Bodi
ya Filamu nchini imewahamasisha watanzania kuongera ari ya kuzipigia
kura filamu za kitanzania zinazowania tuzo za Africa Magic Viewers
Awards (AMVA 2017) za nchini Nigeria.
Katibu
Mtendaji wa bodi hiyo, Bi Joyce Fissoo (pichani juu) ametoa hamasa hiyo
hii leo, wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power Break Fast On
Saturday kinachoendeshwa na watangazaji Philip Mwihava na Godfrey
Kusolwa.
“Filamu
hizo ni Naomba Niseme, Aisha na Home Coming ambazo zinawania tuzo za
filamu bora na Siri ya Mtungi ambayo inagombea filamu bora ya lugha ya
Kiswahili. Niwaase Wanzania, ushindi wa filamu hizi ni sisi kuwapigia
kura hawa vijana wetu ambao wameshika bendera yetu kwenda kutuwakilisha
kule Nigeria, niwasihi waweze kuzipigia kura na wahakikishe
wanahamasisha marafiki zao pia kuzipigia kura ili nafasi zote tuzo zije
Tanzania”. Amesisitiza Fissoo.
Naye
Mtayarishaji wa filamu nchini, Staphord Kihole (pichani) ambaye pia
alikuwa kwenye kipindi hicho, ametumia fursa hiyo kuwaomba watanzania
kuzipigia kura filamu za kitanzania ili zishinde tuzo za Africa Magic
Viewers Choice Awards ikiwemo filamu yake ya "Naomba Niseme" inayowania
vipengele viwili, kikiwemo kipendele cha Best East Africa na Best All
Africa kinachoamuliwa na majaji.
Ili
kuzipigia kura filamu za Tanzania ambazo ni Naomba Niseme, Aisha na
Home Coming, unapakua Application ya We Chat, unajisajiri kwenye Africa
Magic kwa kutumia nambari ya simu na kisha unatafuta kipengele cha AMVCA
na utaweza kupiga kura kadri upendavyo ambapo mtu mmoja anaweza kupiga
kura hadi 100 kwenye filamu tofauti tofauti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...