Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala ameitaka mamlaka ya uhamiaji kuharakisha kufanyia Uchunguzi kwa kaya 180 ambazo zilibainika kuwa na baadhi ya wakuuu wa kaya wanadhaniwa kuwa ni wahamiaji haramu walioingizwa kwenye mpango wa kusaidia kaya maskini TASAF kinyume cha sheria.

Pia kanali Ndagala aliwataka Wanufaika na walengwa wa TASAF Kutumia fedha wanazo zipata kuanzisha miradi midogomidogo itakayo wasaidia kutoka katika wimbi kubwa la umasikini, na kuacha kutumia fedha hizo kinyume na utaratibu uliokusudiwa kwa kufanyia mambo ya anasa.

Kauli hiyo alitolewa jana wakati wa ziara yake vijijini ya kutembelea wanufaika wa Mradi huo katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga, ambapo alisema lengo la serikali kuanzisha Mfuko huo ni kusaidia Watanzania wanaoishi katika Mazingira magumu waweze kupata fedha za kuwapeleka Shule watoto, kupata chakula milo mitatu kwa siku na kuboresha afya zao na kuanzisha miradi itakayo wasaidia kujikwamua na umasikini.

Alisema katika uhakiki uliofanyika wa kuhakiki watu wasio stahili kuwemo katika mradi huo, iligundulika kwa Wilaya ya Kakonko kuna baadhi ya kaya 180 zinazo nufaika na mradi huo ambapo baadhi ya wakuu wa kaya hizo mmoja wao ni Raia kutoka Nchi ya Burundi wanao endelea kunufaika na mradi kinyume na utaratibu uliowekwa kwa Wanufaika wa Mradi huo.

Ndagala alisema kuwahudumia wahamiaji haramu kwenye mpango wa TASAF ni kuhujumu uchumi wa serikali , endapo itagundulika Watu hao tunao wadhania sio raia ikithibitishwa na Maafisa wa Uhamiaji Watatakiwa kurudisha fedha zote walizo kwisha kuzichukua na kwa Wale wajumbe wa Kijiji walio shiriki kupitisha majina yao yaingizwe kwenye mradi watatakiwa kuchukuliwa hatua .

"Leo nimepita mimi mwenyewe kujionea Wanufaika wa Mradi wa TASAF na nimebaini mambo machache, moja wapo ni wahamiaji haramu kuingizwa kwenye mpango, Wanufaika kutumia fedha kama inavyo takiwa wengi wao wanatumia kunywea pombe, na mambo mengine. nimekuja kuwahamasisha watumie fedha hizo kwa kuwajenga kiuchumi na kwa wale walio bainika kwenye uhakiki majina tumeyafikisha kwa idara ya uhamiaji waweze kufanya upembuzi yakinifu ili kubaini uraia wao",alisema Kanali Ndagala.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala  akisalimiana na mmoja wa wanakijiji cha Nyabibuye,wakati Ndagala alipofanya ziara yake kutembelea wanufaika wa Mradi wa TASAF,katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga
 MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala  akimsikiliza mmoja wa wanakijiji cha Nyabibuye,aliyenufaika na mradi wa Kaya Masikini wa TASAF,wakati  alipofanya ziara yake kutembelea wanufaika wa Mradi wa TASAF,katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga.
 Baadhi ya Wanakijiji cha Nyaronga wakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala  (hayupo pichani) wakati alipofanya ziara yake kutembelea wanufaika wa Mradi wa TASAF,katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...