*Ni wale waliohusika na upotevu wa sh. milioni 700
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw. Christopher Ole Sendeka kuwachukulia hatua watumishi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa waliohusika na upotevu wa fedha za maendeleo.
Amesema
zaidi ya sh. milioni 700 zilizopelekwa katika halmashauri kwa ajili ya
miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo sh. milioni 300 za ujenzi wa
Ofisi ya Halmashauri hiyo.Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Januari 26, 2017) wakati
akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
uwanja wa Halmashauri alipokuwa katika ziara yake katika Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.
“Mkuu
wa Mkoa watu wote waliohusika na upotevu huu watafutwe popote walipo na
kuchukuliwa hatua na kisha nipewe taarifa ya hatua ulizochukua.
Hatuwezi kuwavumilia watu hao ambao wanachora ramani kwa sh milioni 200 na sh. milioni 100 zingine hazijulkikani zilipo,“ alisema.
Pia Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu huyo wa Mkoa kufuatilia
kiasi kingine cha sh milioni 400 zilizopelekwa wilayani hapo kwa ajili
ya maendeleo ambazo nazo hazijulikani zilipo. “Tafuta waliohusika popote
walipo hata kama ni nje ya Njombe waje kutueleza ziliko fedha zetu,”
Mbali
na kutoa agizo hilo kwa Mkuu wa Mkoa, pia Waziri Mkuu ameuagiza uongozi
wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) kuhakikisha
inashirikiana nayo inafanya uchunguzi ili kubaini watu waliohusika na
upotevu huo.Katika hatua nyingine,
Waziri Mkuu alisema Serikali haitowavumilia watumishi wote
wanaojihusisha na vitendo vya ubadhilifu wa fedha za umma, hivyo
amewataka watumishi wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na maadili.
Waziri
Mkuu aliwataka watumishi wa umma nchini kuacha tabia ya kudokoa fedha
za maendeleo zinazopelekwa katika Halmashauri zao kwa sababu Serikali
iko macho na itawashughulikia wote watakaobainika kujihusisha na vitendo
hivyo.Aidha,
Waziri Mkuu alitoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini
kusimamia vizuri fedha za maendeleo zinazopelekwa kwenye maeneo yao na
kuhakikisha zinatumika kama ilivyokusudiwa.
Awali
akiwa njiani kuelekea Ludewa Mjini akitokea katika kata ya Mundindi
Waziri Mkuu alisimamishwa na wananchi wa kijiji cha Mlangali ambao
waliiomba Serikali iwasaidie kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali
zinazowakabili ikiwemo ya maji.Mwenyekiti
wa kijiji hicho Bw. Michael Lameck alisema alimueleza Waziri Mkuu
kwamba awali walikuwa wanapata maji ila kwa sasa hayatoki kutokana na
uchakavu wa miundombinu hali iliyowafanya kuchangishana na kupata sh.
milioni 95 kati ya 200 zinazohitajika.
Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu alimuagiza Mhandisi wa Maji wa Wilaya hiyo, Bw. Nasib Mlenge kwenda kijijini hapo leo Januari
27 kukutana na Bw. Lameck ili kushirikiana naye na kuangalia alipofikia
na kuendeleza uboreshaji wa miundombinu hiyo ili wananchi hao wapate
maji.
“Mwenyekiti
amechangisha sh. milioni 95 na kununua baadhi ya vifaa nyinyi
mnashindwa nini. Lazima muwe makini na matatizo ya wananchi na Serikali
haitaki masuala ya urasimu. Watu wana shida ya maji na mnajua tatizo
mmekaa tu,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JANUARI 27, 2017.
Wananchi wa kijiji cha Lusitu wilayani Ludewa wakilizuia gari la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakimtaka asimame na kuwasalimia alipokuwa akienda mjini Ludewa kutoka mgodi wa chuma wa Liganga Januari 26, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alisimama na kuwahutubia.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Lusitu wilayani Ludewa walioziba barabara wakitaka asimame na kuwasalimia alipokuwa akitoka kwenye mgodi wa chuma wa Liganga kwenda mjini Ludewa Januari 26, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa dini baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Halmashauri, mjini Ludewa Januari 26, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...