Kiungo wa zamani wa Real Madrid, Arsenal na Monaco Emmanuel Adebayor anatajwa kuwa
muda wowote kuanzia sasa atajiunga na klabu ya Yanga ya Dar es salaam kwa mkataba mnono.
Taarifa zilizotufikia zinamtaja nahodha huyo wa timu ya Taifa ya
Togo kuwa atajiunga na timu hiyo hili waweze kutetea ubingwa na kujiandaa na
michuano ya kimataifa ya klabu bingwa Afrika.
Adebayor anataka kujiunga na wana-Jangwani hao ikiwa ni siku
chache baada ya timu yao ya Taifa ya Togo kutolewa katika michuano ya AFCON.
Adebayor kama atajiunga klabu hiyo ya Yanga atakuwa mchezaji wa
kwanza kutoka ligi ya mabingwa ulaya kuja kucheza katika ukanda huu wa Afrika
Mashariki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...