Diwani wa Kata ya Sandali, Abel Tarimo (wa pili kulia) akimkaribisha mgeni Rasmi ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilungule na Mkurugezi wa Yamoto Bend, Said Fella (kulia) wakati akiwasili katika hafla ya ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto uliofanyika Kata ya Sandali Dar es Salaam jana kabla ya ufunguzi huo.
Afisa Maendeleo Kata ya Sandali, Anuciatha Kayombo akizungumza jambo katika hafla ya ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto uliofanyika Kata ya Sandali Dar es Salaam jana.
Diwani wa Kata ya Sandali, Abel Tarimo (wa pili kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto uliofanyika Kata ya Sandali Dar es Salaam kabla ya ufunguzi huo na kupata nafasi ya kumkaribisha mgeni rasmi, kuanzia kulia ni Afisa Maendeleo Kata ya Sandali, Anuciatha Kayombo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali, Engerasia Lyimo na kushoto ni Diwani ya Kata ya Kilungule, Said Fella
Mgeni rasmi, Diwani ya Kata ya Kilungule Saidi Fella (kushoto) akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa hafla ya ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto, wakwanza kulia ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali, Engerasia Lyimo na Diwani wa Kata ya Sandali, Abel Tarimo
Diwani Fella katika picha ya pamoja na kikundi cha ngoma cha Hisia Theater Group.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...