Donald Trump akiapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani, akichukua hatamu kutoka kwa Rais Barack Obama saa mbili usiku kwa muda wa Afrika Mashariki. Wafuasi wake walikusanyika kwa wingi barabara za Washington kumshangilia.

Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump pamoja na familia yake wakifurahia mara baada ya kumaliza kuapishwa kwa rais mpya wa Marekani.
Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump akihutubia taifa kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa Taifa hilo. Amerudia ahadi yake ya kampeni ya kuifanya nchi yake kuwa taifa lenye nguvu zaidi kuliko hapo awali, huku maelfu wakiandamana nchini Marekani kupinga kuapishwa kwake.

Taswira ya wananchi waliohuhudia kuapishwa kwa Donald Trump
Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump (mwenye tai nyekundu) akimsindikiza Rais aliyemaliza muda wake Barack Obama pamoja na aliyekuwa Makamu wa rais wake
Rais wa Marekani Donald Trump akipeana mkono na Rais aliyemaliza muda wake Barack Obama

Rais aliyemaliza muda wake Barack Obama akiwapungia mkono
Helikopta iliyombeba rais aliyemaliza muda wake Barack Obama pamoja na mke wake ikiondoka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...