Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassana ameishukuru Serikali ya India kwa ufadhili wake wa miradi ya maji katika miji 17 nchi ambayo inalenga kupunguza tatizo la maji kwa wananchi wengi nchini.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 68 ya Siku ya Kitaifa ya Jamhuri ya India sherehe ambazo zimeambatana na Uzinduzi rasmi wa majengo ya ofisi mpya ya Ubalozi wa India hapa nchini.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema ufadhili wa miradi ya Maji pamoja na miradi mingine unaofanywa na Serikali ya India kwa Tanzania Bara na Zanzibar unadhihirisha wazi mahusiano mazuri yaliyopo yaliyoasisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mahatma Gandhi wa India.
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa India ni moja ya washirika muhimu katika juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo na Serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu katika maeneo mengi ikiwemo ya kikanda na kimataifa kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande Mbili yaani Tanzania na India.
Amesema kwa miaka mingi sasa mahusiano ya kindugu yamekuwa yaakiimarika katika sekta mbalimbali ikiwemo kisiasa,kidiplomasia,kibiashara, masuala ulinzi, utamaduni na mwingiliano wa watu na watu. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo jipya la Ubalozi wa India lililopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam mbele ya Balozi wa India Bw. Sandeep Arya .
Balozi wa India hapa nchini Bw. Sandeep Arya akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan picha mbali mbali zenye kuonyesha historia ya urafiki baina ya Tanzania na India wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la ubalozi wa India jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Jengo jipya la Ubalozi wa India hapa nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Jengo jipya la Ubalozi wa India lililopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Sasa serikali inahamia Dodoma nyie munajengo ofisi za ubalozi mpya dar?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...