Na Woinde Shizza,Arusha
Jeshi la polisi mkoani hapa kwa kushirikiana na tume ya kuratibu na kudhibiti dawa za kulevya nchini limeteketeza magunia 58 ya bangi,mbegu za bangi kg 210 huku hekari 19 zilizooteshwa miche ya bangi zikiwa zimeharibiwa .
Hayo yamebainishwa leo na kamanda wa polisi mkoani Arusha,Naibu Kamishna wa polisi Charles Mkumbo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa kuteketeza kwa madawa haya ya kulevywa kumefanyika kutokana na operationi ya siku mbili .
Alisema kuwa operesheni ya kwanza ilofanyika january 10 siku ya jumanne kuanzia muda wa saa 11.00 alfajiri katika eneo la kijiji cha kisimiri juu ndani ya kata ya uwiro tarafa ya kingori na kufanikiwa kupata magunia 31 pamoja na mbegu kilogramu 210 ambazo zote ziliteketezwa na moto ,pamoja na hekari 19 zilizooteshwa miche ya bhangi ambazo ziliaribiwa zote.
Aliongeza kuwa operesheni hiyo iliendelea tena siku ya alhamisi january 12 kuanzia muda wa saa 11.00 alfajiri hadi saa saba mchana katika eneo la kijiji cha Engalaon kata Mwandeti tarafa ya Muklati ambapo walikamata jumla ya magunia 27 ya bangi na kuyateketeza na moto na kuharibu jumla ya hekari 12 zilizooteshwa mmea wa bhangi .
Mkumbo alisema kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama linaendelea na operationi hii hasa ya kuaribu mimea ya bangi mara kwa mara hasa katika cha mvua hali ambayo itasaidia kuthibiti kilimo hicho.
Aidha pia jeshi la polisi linawaonya viongozi wa maeneo yanayohusika na kilimo cha bangi kuacha mara moja kuwaunga mkono wakazi wa maeneo hayo, kwani matukio hayo yanafanywa kwa uwazi bila wao kuchukua hatua yeyote ,wanapaswa watambue kwamba wao ni walinzi wa maeneo yao ,na kuwasihi viongozi washirikiane kwa pamoja kutokomeza kilimo hicho cha bhangi ambayo inaleta madhara makubwa kwa jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...