Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa katika hali ya kuamsha hari na morali ya kufanya kazi kwa watendaji wa Jeshi la Magereza amefanya ziara ya kikazi katika baadhi ya Magereza ya Mkoa wa Morogoro na Pwani mwishoni juma hili.

Ziara hiyo imejumuisha Magereza ya Mbigiri, Wami Kuu, Wami Vijna, Mahabusu, Kihonda, Kingolwira Complex yote ya mkoa wa Morogoro na Shule ya Sekondari Bwawani na gereza Ubena vya mkoani Pwani.

Kutoka kwa Kaimu Jenerali maafisa na askari aliwapata taarifa fupi ya Uwekezaji wa Ubia katika kiwanda cha sukari cha gereza Mbigiri Mkoani Morogoro kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF na NSSF. Alisema uwekezaji huu ni kwa faida ya Jeshi kama Taasisi hivyo ni vizuri kila askari akalifahamu hilo.

Katika ziara hiyo pia alipata wasaa wa kufanya vikao na watendaji ambapo maafsa, askari na watumishi raia walipata fursa ya kuuliza maswali moja kwa moja kutoka kwa Mtendaji mkuu wa Jeshi la Magereza ambapo baadhi ya mambo yalipatiwa majibu ya papo hapo na mengine kupewa ahadi ya kutatuliwa katika siku za usoni hasa yenye uhusiano na masuala ya kibajeti.

Miongoni mwa masuala yaliyoonekana kuwa ni tatizo sugu ni pamoja na huduma za maji, usafiri, matibabu kwa wafungwa na mahabusu, sare za askari, posho mbalimbali kulingana na stahiki ya kila askari na mambo mengine madogo madogo ambayo yote kimsingi yanagusia suala la fedha.

Katika vikao hivyo Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa alitolea maelekezo baadhi ya mambo yaliyohitaji kauli ya Makao Makuu ya Jeshi lakini pia aliwahakikishia kuwa ofisi yake itaendelea kushughulikia kero zote na kusaidia kwa haraka pale inapohitaji kwa kutegemeana na hali ya fedha kwa wakati huo.

Kaimu Kamishna Jenerali aliwaasa maafisa askari kuwa waangalifu wanapotumia mitandao ya kijamii hasa kwa kuzingatia viapo vya utumishi wao.“Ninyi ni askari wenye viapo vya utii wa mamlaka zilizopo, jiepusheni na mijadala ya mitandaoni kwani mingine iko kinyume na maadili ya kazi zetu. Ukipokea ujumbe usiofaa futa kabisa badala ya kuusambaza” alisisitiza Dr. Malewa
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (wa kwanza kulia) akitembelea jengo la Karakana ya Ufundi ya Gereza Wami Vijana. Jengo hilo pamoja na kuendelea kutumika lakini bado linahitaji kukamilishwa kujengwa na kuwekewa miundombinu ili liweze kutoa huduma kama ilivyokusudiwa.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akipata maelezo mafupi ya kiutendaji kutoka kwa Mkuu wa Gereza la Mahabusu Mrakibu wa Magereza (SP) Zephania Neligwa (aliyesimama) ofisini kwake wakati wa ziara ya Kaimu Kamishna Jenerali Mkoani Morogoro aliyoifanya mwishoni mwa juma.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (wa kwanza kushoto) akikagua maendeleo ya jengo jipya la ofisi ya Mkuu wa Gereza Kihonda. Jengo hilo linashengwa kwa jitihada za Mkuu wa Gereza hilo kwa kushirikiana na maafisa na askari wa kituo hicho. Viongozi wengine hapo ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Mzee Nyamka, Mkuu wa Shirika la Magereza (Corporation Sole) Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Joel Bukuku na Mkuu wa Gereza Kihonda Kamishna Msaidizi wa Magereza Ben Mwansasu.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akiendelea kusikiliza hoja mbalimbali za maafisa na askari wa Gereza Kihonda wakati wa ziara ya kikazi kituoni hapo. Aliyesimama ni Mkaguzi Msaidizi wa Magereza (A/Insp) Amani Moses akichangia jambo wakati wa kikao hicho
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akikagua maendeleo ya moja ya nyumba za zinazojengwa kwa mtindo wa kujitolea katika gereza la Wanawake Kingolwira mkoani Morogoro ikiwa ni jitihada za kukabiliana na tatizo la uhaba wa nyumba kituoni hapo. Aliyefuatana naye ni Mkuu wa Gereza la Wanawake Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Loyce Luhembe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...