Mabingwa
watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga wamefanikiwa kukaa kileleni
mwa msimamo wa ligi baada ya kutoka na ushindi wa goli 2-0 kwenye
mchezo uliofanyika leo katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
salaam.
Obrey Chirwa aliyeingia dakika ya 62 akichukua nafasi ya
Haruna Niyonzima alikuwa nyota wa mchezo huo kwa kuifungia timu yake
goli 2 katika dakika ya 69 na 82.
Yanga waliingia uwanjani
wakitafuta ushindi wa aina yoyote ambapo mpaka kipindi cha kwanza
kinamalizika timu hizo zilienda mapumziko wakiwa hawajafungana.
Mwadui
waliokuwa makini katika safu yao ya ulinzi waliweza kuwadhibiti
washambuliaji wa Yanga na kuwafanya kushindwa kupata goli la mapema.
Kila
upande walifanya mabadiliko kwa ajili ya kusaka ushindi huo, na baada
ya matokeo haya Yanga anaongoza ligi akiwa na alama 46, akifuatiwa na
Simba mwenye alama 45 huku Azam akiwa na alama 34.
Wachezaji
wa Timu ya Mwadui, wakiusindikiza mpira kwa macho wakati ukiingia
wavuni, baada ya kupigwa kwa umaridadi mkubwa na Mshambuliaji wa Yanga,
Obrey Chirwa na kuipatia timu yake goli la kuongoza.
Mshambuliaji
wa Yanga, Obrey Chirwa na Simon Msuva wakishangilia ushindi wao dhidi
ya Mwadui Fc, katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara, uliopigwa jioni
hii katika Dimba la Taifa, jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda 2-0.
Furaha ya ushindi kwa wachezaji wa Yanga.
Mshambuliaji
wa Yanga, Amis Tambwe akiwania mpira na Beki wa Mwadui, Nassor Chollo,
wakati wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara, uliopigwa katika Dimba la
Taifa, jijini Dar es salaam leo. Yanga imeshinda goli 2-0.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...