Taja jina la Bitebo popote ulipo tanzania, na hata dunia nzima kwa jumla, na dhana ya utaalamu wa kunyoa nywele inamjia yeyote anayelisikia. Unajiuliza, je ni kwa nini jina hilo limekuwa maarufu hivyo hadi inashangaza? 
Globu ya Jamii ilitembelea kiwanda cha kutengeneza mitindo ya nywele cha New Bitebo Hair Designer maeneo ya Magomeni Mikumi, jirani na ukumbi maarufu wa Lango la Jiji jijini Dar es salaam na kukutana na Mkurugenzi Mtendaji na mmiliki wa kiwanda hicho – Abdallah Bitebo ambaye badala ya kutuambia ni nini siri ya mafanikio yake akaamua kututembeza kiwandani humo ili kujionea wenyewe. 
"Sera ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ni ya viwanda. Nasi hapa tunamuunga mkono kwa kuwa na kiwanda cha kutengeneza mitindo ya nywele na ndevu za watu kwa weledi wa kimataifa. 
"Mzee Magufuli kila siku unamsikia kiwanda sio lazima kikwe kikuuubwa, bali hata cha chumba kimoja ni kiwanda. Sembuse ya sisi hapa ambapo tuna nyumba nzima", amesema Bitebo ambaye kiwanda chake hutembelewa sana na nyota wa tasnia mbalimbali ikiwemo filamu, soka na muziki na hata wa dini na siasa. 
 Hakika anastahili sifa zote hizo na zaidi. Na si ajabu kiwanda hicho kikachaguliwa kwa kura nyingi mno na kutwaa tuzo ya kuwa Best Hair Designer wa Tanzania mwaka 2016. Jionee mwenyewe…
Bango lililopo nje ya kiwanda cha kutengeneza mitindo ya nywele cha New Bitebo Hair Designer maeneo ya Magomeni Mikumi, jirani na ukumbi maarufu wa Lango la Jiji jijini Dar es salaam 
Mkurugenzi Mtendaji na mmiliki wa kiwanda hicho Abdallah Bitebo (kati) akiwa na jeshi lake la kazi
Mkurugenzi Mtendaji na mmiliki wa kiwanda hicho Abdallah Bitebo (kati) akiwa na jeshi lake la kazi
Mteja akipigwa scrub ya nguvu katika kiwanda cha kutengeneza mitindo ya nywele cha New Bitebo Hair Designer. Wenyewe wanakwambia unaingia mzee unatoka kijana. Ukiwa kijana unatoka mtoto...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...