Na Bashir Yakub.
Yafuatayo ni maneno/taarifa/maudhui ya msingi yanayotakiwa kuwa kwenye
wosia . Taarifa yoyote kati ya hizi ni ya muhinu na inacho kitu cha msingi
na cha kisheria inachosimamia na kulinda. Maana yake ni kuwa kukosekana
kwake kutaathiri wosia wako kwa namna moja au nyingine.
( a ) Anza kwa kuandika kichwa( heading). Kichwa utaandika kawaida kama
unavyoandika kichwa cha barua au taarifa nyinginezo.
Mfano “WOSIA” au “ WOSIA WANGU MIMI PASCHAL STEVEN MUTIGANZI”,
vyovyote kitakavyoandikwa muhimu kiwepo kichwa.
( b ) Kinachofuata baada ya kichwa ni sentensi muhimu sana. Ni sentensi
inayolenga kuondoa utata mbeleni.
Mfano ; “ HUU NI WOSIA WANGU NA WA MWISHO MIMI PASCHAL STEVEN
MUTIGANZI”.
Ni sentensi inayoazimia kuwa hakuna wosia mwingine baada ya huo. Ni
sentensi inayolenga kufuta/kuondoa aina yoyote ghushi.
( c ) Kinachofuata ni kipengele ambapo mtoa wosia/mwandika wosia
anajitambulisha kwa majina kamili, anuani na tarehe ya kutoa/kuandika
wosia. Anuani ijieleze vizuri. Isiwe tu P.O. BOX… ikaishia hapo. Ieleze namba
ya nyumba kama ipo, mtaa, kata, wilaya na mkoa. Na anuani nzuri ya
kuweka ni ile ya pahala yalipo makazi yako ya kudumu wewe mtoa wosia.
Ikiwa unayo makazi mawili ya kudumu kwa wale wa mitala basi chagua
mojawapo.
Mfano: “WOSIA HUU UMEANDIKWA LEO TAREHE 13 / 2 / 2017 NA MIMI
PASCHAL STEVEN MUTIGANZI WA NYUMBA NAMBA 13 , MTAA WA
MWINJUMA, KATA MWANAYAMALA , WILAYA YA KINONDONI, MKOANI DAR
ES SALAAM, wa S.L.P 100 .
( d ) Andika sentensi ya kuvunja wosia nyingine zilizopita. Hii ni pale
ambapo umeandika wosia mpya na kufuta ule wa nyuma. Lakini hata kama
haujawahi kuandika wosia ila sasa ndio unaanza basi hakuna ubaya pia
ukiweka sentensi hiyo.
Mfano ; “WOSIA HUU UNAFUTA WOSIA NYINGINE ZOTE NILIZOWAHI
KUTOA/KUANDIKA HUKO NYUMA”.
( e ) Kinachofuata ni kipengele kinachotaja orodha ya mali ulizonazo. Habari
si tu kutaja mali, bali pia ni kuzichambua mali hizo na kutaja pahala zilipo
kila moja. Mali utazitaja kwa namba. Namba 1….2……3…..n.k.
Mfano ; “JUMLA YA MALI NILIZONAZO NI, 1. NYUMBA NAMBA 13 , ILIYOPO
MTAA WA MWINJUMA, KATA MWANAYAMALA , WILAYA YA KINONDONI,
MKOANI DAR ES SALAAM. 2. GARI…..”( taarifa za gari au mashine yoyote
zitajwe kama ilivyo kwenye kadi yake ya usajili)……( endelea kutaja mali )
( f ) Kinachofuata ni kipengele kinachotaja orodha ya warithi/wanufaika wa
mirathi. Wataje kwa majina yao yote.
Mfano; “WARITHI WANGU KATIKA WOSIA HUU NI
1………………………..2……………………………3…………………..”n.k.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...