Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemtumia
salamu za pole na pongezi Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel
Kyunga kwa kazi nzuri na kubwa waliyoifanya ya kuwaokoa wachimbaji wadogo 15
waliofukiwa na maporomoko ya udongo kwenye Mgodi wa Dhahabu wa RZU uliopo katika
Kijiji cha Nyarugusu, wilaya ya Geita katika mkoa wa Geita.
Tukio hilo
la kufukiwa wachimbaji hao wadogo 15 wakiwemo Watanzania 14 na Raia Mmoja wa
China lilitokea usiku wa Tarehe 26 Januari mwaka 2017.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema
amepokea kwa furaha taarifa za kuokolewa kwa wachimbaji hao wadogo na amesifu
na kupongeza jitihada za kuwaokoa wachimbaji hao zilizofanywa na Serikali ya Mkoa wa Geita,
Jumuiya ya Wachimbaji Wadogo wa mkoa wa Geita, Wamiliki wa Migodi ya Dhahabu na
wananchi kwa ujumla kwa kutoa vifaa mbalimbali vya uokoaji jitihada ambazo zimepelekea
kuokolewa kwa wachimbaji hao wakiwa hai.
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa “jitihada
,Umoja na Mshikamano ulioonyeshwa na makundi mbalimbali katika kuwaokoa ndugu
zetu waliofukiwa na maporomoko ya Udongo wakiwa kazini huko Geita ni mfano mzuri
na wakuigwa na wananchi na taasisi nyingine nchini katika kujitolea kwa hali na
mali hasa vifaa vya uokoaji kwa ajili ya kusaidia watu wanaopatwa na majanga
ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea kama walivyofanya ndugu zetu wa mkoa wa
Geita nawapongeza Sana”.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan
amewataka wamiliki wa migodi kote nchini wahakikishe wanafanya kazi zao za
Kupitia
kwako Mkuu wa mkoa wa Geita napenda kutuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na
marafiki kufuatia kutokea kwa tukio hilo na nawaombea kwa Mwenyezi Mungu
wachimbaji hao ambao kwa sasa wanapatiwa matibabu Katika Hospitali ya Serikali
ya mkoa wa GEITA matibabu mema ili waweze kupona haraka na kurejea kwenye kazi
zao za kujitafutia riziki.
Wakati huo
huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kitengo cha Kudhibiti Maafa nchini, Wizara ya Nishati na Madini pamoja na
Wizara ya Mambo ya Ndani kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kwa Ofisi ya Mkuu wa
mkoa wa Geita na kupekelea kuchukuliwa hatua za haraka katika kushughulikia
ajali hiyo.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dar es Salaam
29-Jan-2017.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...