Mabingwa wa soka barani Afrika
Mamelodi Sundowns FC ya Afrika Kusini wanatarajiwa kuwasili nchini mwisho wa
mwezi huu kwa mwaliko wa klabu ya African Lyon.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi
wa African Lyon, Rahim Kangezi, Mamelodi
wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam Januari 30, 2017 na kucheza michezo
miwili ya kirafiki na Simba SC na Yanga.
“Mamelodi wanakuja Tanzania
kuiunga mkono Tanzania katika kampeni yake ya “LINDA TEMBO WETU” ambayo ni
mahususi kupiga vita ujangili na biashara haramu ya pembe za tembo.
Kangezi amesema mchezo wa
kwanza Mamelodi watacheza na February 1, 2017 na Simba na February 3, 2017
watachuana na Yanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...