Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) imepata tuzo kutoka Umoja wa Afrika
(AU) kutokana na mfumo wa Uondoaji Mizigo Bandarini (TANCIS) ambao unafanya
kazi kwa ufanisi na uharaka zaidi pamoja na kudhibiti mianya ya rushwa.
Tuzo hiyo imetolewa na Umoja wa Nchi za Afrika
jijini Addis Ababa Ethiopia, baada
ya kufanyika shindano la Taasisi za Serikali za Umoja wa Nchi hizo kutokana na kuboresha mifumo ya utendaji
kazi katika taasisi zao.
Akizungumza
kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi.
Mindi Kisiga amesema kuwa TRA na Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii (SSRA) ndiyo taasisi pekee za Serikali zilizoweza kufanya vizuri katika
ubunifu katika utendaji wa taasisi hizo.
“Tuzo hizi
zinatolewa na nchi za Umoja wa Afrika kwa taasisi za Serikali ambapo
hushindanishwa katika masuala ya ubunifu katika utendaji kazi wa taasisi husika,”
alisema Bi. Mindi.
Akizungumza
kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
toka Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Richard Kayombo alisema TRA imeshinda tuzo
hiyo kutokana na ubunifu wa mfumo wa TANCIS ambao umeundwa kwa kuzingatia
kanuni za hali ya juu za kiteknolojia kwa lengo la kuongeza ufanisi, uharaka,
uwazi na uhakika katika usimamizi wa masuala ya forodha.
Meneja Mifumo ya Kielektroniki ya Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tinkasimile Felix (kushoto) akipokea tuzo ya ubunifu wa mfumo wa TANCIS kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasilianokutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga. Mfumo huu wa TANCIA umeundwa kwa kuzingatia kanuni za hali ya juu za kiteknolojia kwa lengo la kuongeza ufanisi, uharaka, uwazi na uhakika katika usimamizi wa masuala ya forodha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...