
MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amewataka Madaktari ,wauguzi pamoja na watoa huduma za afya katika Hospitali Vijibweni kutumia taaluma yao vizuri ili kuwawezesha wananchi wa eneo hilo kupata huduma nzuri.
Meya Isaya ametoa ushauri huo jijini Dar es Salaam jana katika hafla iliyoandaliwa na wauguzi wa Hospitali hiyo iliyopo Wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati walipokuwa wakiuwaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017.
Katika hafla hiyo pamoja na mambo mengine Meya Isaya alisisitiza kwamba kila mmoja anapaswa kufanya kazi kwa upendo kwani kazi yao ni yawito kuliko sekta nyingine.
Alisema wananchi wanapopata huduma nzuri hupata faraja lakini wanapokumbwa na misukosuko kwa watoa huduma sio jambo zuri kwani unaweza kumuongezea mgonjwa maradhi mengine na hivyo akawasihi wafanye kazi zao kwa upendo.
“ Niko pamoja na nyinyi, najua kazi yenu hii ni yawito, lakini mnaposhindwa kufanya kama ambavyo imekusudiwa hili ni tatizo, kwanini mpate sifa mbaya katika huduma yenu?” aliuliza Meya Isaya.
Awali akisoma risala Dokta wa hospitali hiyo, alisema kwamba Hospitali hiyo inatoa huduma za rufaa kwa Kata za vijibweni ,Mjimwema, Kigamboni, Tungi, Somangila, Kibada na maeneo yote ya manispaa ya Kigamboni ambapo kwa sasa hospitali hiyo ndio inayofanya kazi za hospitali ya Wilaya katika manispaa ya Kigamboni.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...