Mkuu wa wilaya ya Mbinga Mhe. Consimas Mshenyi (pichani) amewataka wananchi wilayani humo kuhakikisha wanatunza ziada ya chakula walichonacho kutokana na hali ya mvua kutoridhisha  licha ya kusema hakuna njaa katika wilaya yake.

Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari kuhusu hali ya chakula katika wilaya hiyo mkuu huyo wa wilaya amesema mpaka sasa vituo vya hifadhi ya chakula wilayani hapo vina zaidi ya tani 300 huku ziada kutoka kwa wananchi ikiwa ni tani 10,000 za mahindi huku mchele ikiwa ni tani 18,000.

 “Nawataka wananchi waendelee kuhifadhi ziada ya chakula walichonacho kwani hali ya mvua si nzuri na ziada hiyo inaweza kupungua pia ziada hiyo inaweza saidia hata kwa majirani zetu” alisema DC Mishenyi.

Aidha Mhe. Mishenyi alisema kuwa hali mazao yaliyopo shambani yapo katika hali nzuri licha ya mvua kunyesha katika hali ya kutoridhisha lakini kuna uhakika wa mazao hayo kukomaa na kuvunwa kwa wakati hivyo akawataka wananchi hususani wakulima kuhakikisha wasimamia utanzaji kwa kushirikiana na wataalamu wa kilimo
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amepiga marufuku unywaji na uuzwaji wa pombe nyakati za kazi kwani kunazoletesha maendelea ya nwilaya hiyo “sitawavumilia wanaokunywa saa za kazi na wanaocheza pool table  nyakati za mchana yaani saa za kazi nitawamuagizaa kupitia kwa afisa biashara mkurugenzi kufuta leseni kwa wale vwote watakao kiuka mashart ya biashara zao ikiwemo kuuza pombe katika saa za kazi”

Kuhusu uchaguzi mdogo wa udiwani utakaofanyika Januari 22 mwaka huu  katika kata ya maguu wilayani hapa Mishenyi amewataka wanachi kupiga  kura kwa amani na kurejea makwao kusubiri matokeo, huku akiwaomba wagobea kutokuwa vyanzo kuvuruga amani na utulivu na kuwahakikishia ulinzi  wa kutosha katika uchaguzi huu 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...