Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 54 nchini Vietnam, Man Van Nhat ameondolewa kifaa cha upasuaji kilichosahahulika wakati wa kufanyiwa operesheni tumboni mwake kwa miaka 18 iliyopita.
Madaktari nchini Vietnam wamekiondoa kifaa hicho cha upasuaji kwa mtu ambae amedumu nacho katika mwili wake pasipo kufahamu kwa miaka 18. Televisheni ya taifa VTV imeripoti kuwa Man Van Nhat, mwenye umri wa miaka 54 amesema kifaa hicho kilisahaulika tumboni mwake mwaka 1998 wakati alipofanyiwa upasuaji wa dharura, uliotokana na ajali ya barabarani.
Kwa mara kadhaa Nnat alikuwa akihisi maumivu ya tumbo na alipokwenda hospitali alipewa dawa za kutuliza vidonda vya tumbo.
Lakini baada ya uchunguzi wa X-ray, ambao ulifanyika mwaka jana ikabainika kuwa mzizi wa maumivu yake kuwa ni kifaa hicho kilichosahaulika tumboni. Kifaa cha urefu wa sentimita 15 kikiwa kimegawanyika baada ya kumeguka kilikuwa kikimsababishia maumivu mtu huyo.
Mkurugenzi wa hospitali ya Back Kan, Trinh Thi Luong, amekiambia kituo cha televisheni cha VTV, kwamba maafisa wapo katika jitihada za kumsaka yule aliyekiacha kifaa hicho katika tumbo la Nhat. Amesema hata kama tayari wamestaafu watawaeleza ili iwe funzo kwa madaktari wengine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...