Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida.
Viongozi,
Watendaji na Watumishi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Singida wametakiwa
kuhakikisha taarifa zote za mapato na matumizi zinawafikia wananchi wote katika
ngazi ya Kata na Kijiji ili waweze kuelewa hasa kiasi cha fedha zilizoingizwa
na Serikali katika Halmashauri na namna zinavyo tumika.
Agizo
hili limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi katika ziara yake
ya kuzitembelea Halmashauri zote za Mkoa huo kwa lengo la kujenga Uelewa wa
pamoja, utumishi wa pamoja, na kasi ya pamoja ili kufikia lengo pamoja kwa
maslai mapana ya Taifa.
Kwa
upande wa Wakuu wa Idara na Vitengo Dkt Nchimbi amewaagiza wawe na taarifa za
kila siku za watendaji na watumishi katika mnyororo wote wa kiutendaji na
kiuongozi na kuepuka kutegemea taarifa za makaratasi na ili kuimrisha utendaji
wa kuzingatia matokeo yanayo onekana.
Niaibu sana kwa Mganga Mkuu wa Wiwala (DM)
kushindwa kutoa takwimu pale unapo ulizwa swali nje ya ofisi yako juu ya idadi
ya watoto waliozaliwa ndani ya siku tatu katika wilaya yako au Afisa Elimu wa
Halamashari unashindwa kutoa jibu la ni Walimu wangapi katika Halmashauri yako
hawakuingia kazini kwa sabau za kiafya. Sinto penda hali hii iendelee
kujitokeza katika Mkoa wa Singida. Aliongeza Dkt Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi (wa pili kutoka kushoto) akishiriki kupalilia zao la mtama Mtama katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akishiriki kupanda Mihogo katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi (wapili kutoka kulia) akishiriki kikamilifu katika shughuli za kilimo katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.
Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akishiriki chakula cha mchana baada ya kukaribishwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mwenge Singida katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...