Ujumbe wa watu watano kutoka Chuo Kikuu cha Tiba cha Minnesota kutoka nchini Marekani leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendajji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru.
Ujumbe huo umeongozwa na Mkuu wa masuala ya utafiti katika Idara ya Magonjwa ya dharura kutoka Chuo hicho, Profesa Michelle Biros .
Katika mazungumzo hayo Profesa Museru ameuleza ujumbe huo mikakati na malengo mbalimbali ambayo MNH inafanya katika kuhakikisha huduma za kibingwa zinafanyika nchini ikiwa ni pamoja na upandikizaji wa figo, kuweka kifaa maalum cha usikivu na kuongeza wodi kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum.
Kwa mujibu wa Profesa Museru, MNH inakabiliwa na changamoto ya wataalam katika baadhi ya maeneo ikiwamo ICU.
Maeneo waliotembelea ni Idara ya Magonjwa ya dharura na Ajali, Idara ya Mionzi, Mwaisela -wodi moja, Jengo la watoto na Jengo la wazazi namba mbili -Wodi 35.
Mmoja wa msimamizi wa wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu wa hospitali hiyo, Trustworthy Majuta akifafanua jambo wa ujumbe huo leo.
Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa Nje, Dk Raymond Mwenesano akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo leo. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...