Msanii wa muziki wa asili nchi, Mrisho Mpoto ambaye pia amekuwa
mmoja kati ya wasanii ambao wanatoa elimu kwa jamii juu ya kukomesha suala la
mauwaji ya tembo nchini, ameipokea kwa furaha hatua ya nchi ya China kutaka
kupiga marufuku biashara ya meno ya Tembo nchini humo.
Mapema Jumamosi hii katika matembezi ya amani ya kupinga
ujangili hapa nchini, Balozi wa China, Lu Youqing alisema nchi ya China ipo
kwenye mkakati wa kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo na wanatarajia
mwishoni mwa mwaka huu biashara hiyo kufa kabisa.
Akiongea na waandishi wa habari kuhusu kauli hiyo, Mrisho Mpoto
alisema hatua hiyo ni nzuri na itasaidia nchi mbalimbali duniani kuiga nyayo
zao.
“Mimi ni mmoja kati ya wasanii ambao tumekuwa tukihusika sana
katika hizi harakati hasa hasa kimataifa zaidi, nimeshasafiri nchi mbalimbali
kama mtanzania kupinga mauwaji ya tembo au ujangili ndio maana hata leo nipo
kwa baada ya kualikwa na ubalozi wa China kwamba wameona jitihada zangu,”
alisema Mpoto.
“Kwa hiyo alichokisema balozi kuhusu nchi ya China kupiga marufuku
biashara ya meno ya tembo ni kitu kizuri sana kwa sababu huu ni mwanzo kwa
China ambao zimekuwa zikisema China ndo vinara wa biashara hiyo kuwa na mtazamo
mwingine, lakini pia kupitia maamuzi haya naona sasa biashara hii inaenda
ukingoni kama nchi zingine za Ulaya ambazo zimekuwa zikitajwa kufuata msimamo
wa China,”
Alisema suala la kupinga ujangili nchini sio suala la mtu mmoja,
kila mtanzania ana haki ya kulinda maliasili za nchi kwajili ya kizazi kijacho.
Pia muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na wimbo Sizonje,
amesema yeye bado ataendeleza mapambano kwa kuanzisha kampeni mbalimbali ambazo
zitawafanya watanzania kufichua majangili kwa kuwa ni watu ambao wanatoka
katika jamii zetu.
Msanii wa muziki wa asili nchi, Mrisho Mpoto akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja.Gen Gaudence Milanzi wakati wa matembezi ya kupinga ujangili unaofanywa dhidi ya Tembo ya kilometa 5 kutoka Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya Sea Cliff ambapo wageni mashuhuli kama Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa alishiriki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...