Mwandishi wa habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru na Mzalendo, Amina Athuman (pichani) amefariki Dunia leo asubuhi katika Hosptali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar alikokuwa amelazwa.
Amina alilazwa Hospitalini hapo baada ya kuzidiwa (kushikwa na uchungu) kutokana na ujauzito na kukimbizwa kupata huduma katika hospitali hiyo ambpo alijifungua mtoto wa Kiume (bahati mbaya) na yeye akaendelea kupatiwa matibabu hadi ulipomkuta umauti leo asubuhi.
Amina alikuwa mjini Zanzibar kikazi alipokwenda kuripoti mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo alikuwa arejee jijini Dar es Salaam jana. Tutaendelea kupeata taarifa, ikiwa ni pamoja na mipango ya mazishi, kwa kadri tutavyozipata.
Mungu ilaze roho ya Marehemu
Amina Athuman mahala pema peponi
- Amina
Amina Athuman mahala pema peponi
- Amina
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...