Kama wewe ni mpenzi wa filamu ya kihindi basi sura ya Mwigizaji huyu mashuhuri nchini India Om Puri, ambaye pia aliigiza kwenye filamu zilizovuma sana nchini Uingereza si ngeni machoni mwako, Mwigizaji huyu amefariki dunia leo Januari 6 akiwa na umri wa miaka 66.

Om Puri aliigiza kwenye filamu ya ucheshi ya East is East nchini Uingereza ambayo ilisimulia kuhusu maisha ya mhamiaji kutoka Pakistan aliyekuwa akizoea maisha ya kaskazini mwa England.

Taarifa zinasema mwigizaji huyo alifariki baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo nyumbani kwake huko Mumbai nchini India.

Om Puri alijulikana sana kwa ustadi na uigizaji wake katika filamu za Kihindi miaka ya 1980.

Aidha, aliigiza kwenye filamu za Kiingereza, zikiwemo Mahatma Gandhi ya Richard Attenborough.

Aliigiza pia katika filamu za Pakistan na Hollywood.
Mwaka 2004, alitunukiwa nishani ya staha ya OBE kwa mchango wake katika tasnia ya filamu Uingereza.

Puri, alizaliwa 1950 jimbo la Haryana, kaskazini mwa India.

Filamu yake ya kwanza kuigiza ilikuwa ya Ghashiram Kotwal mwaka 1976.
nchini India, anafahamika kwa filamu maarufu za Ardh Satya, Sadgati, Paar na filamu ya ucheshi ya Jaane Bhi Do Yaaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...