Mwili wa mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la uhuru na mzalendo Amina Athuman ukisafirishwa asubuhi hii na boti ya kilimanjaro kuelekea Dar es Salaam na kusafirishwa hadi kijijini kwao Lushoto kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya jumanne mchana. Marehemu alikuwa Zanzibar kikazi akiripoti habari za michezo kombe la Mapinduzi na kumkuta mauti hayo baada ya kujifungua mtoto wa kiume, kwa bahati mbaya mtoto akafariki baada ya kuzaliwa na yeye kupata kifafa cha uzazi na kufariki jana asubuhi. Mwenyenzi mungu ampe kauli thabiti na amsamehe madhambi yake-Ameen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Inasikitisha sana, tumewapoteza wote wawili. Lakini pia Wajiri mjifunze kitu, Mama wa watu anakaribia kujifungua anaendaje safari ndefu ya majini? hata kama alienda kwa ndege bado lazima tujali afya ya mama na mtoto.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...