Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson, akipeperusha bendera ya Taifa wakati wa mkesha mkubwa wa kitaifa wa dua maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana. Dk.Akson alimwakilisha Rais Dk.John Magufuli kwenye mkesha huo ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Na Dotto Mwaibale

NAIBU Spika wa Bunge Dk. Tulia Akson amesema Tanzania mpya na yenye matokeo chanya kwa mwaka 2017 inawezekana hivyo akamataka kila mmoja wetu kufanyakazi kwa bidii ili kuliletea taifa maendeleo.

Dk.Akson aliyasema hayo kwa niaba ya Rais Dk.John Magufuli wakati akihutubia kwenye mkesha mkubwa wa kitaifa wa dua maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana.

"Tanzania mpya na nchi mpya yenye matokeo chanya kwa mwaka 2017 inawezekana" alisema Akson.



Akson alimwakilisha Rais Dk.John Magufuli alikuwa mgeni rasmi kwenye mkesha huo mkubwa ulioandaliwa na makanisa mbalimbali ya kiroho.

Akinukuu baadhi ya maneno kutoka katika kitabu cha biblia cha Nyakati mungu ataiponya nchi iwapo kila mtu atamuita kwa jina lake na kujinyenyekesha na kuomba na kuziacha njia mbaya.


"Tukimuita mungu kwa jina lake na kujinyenyekesha kwa kuacha kutenda mambo mabaya mungu ataiponya nchi yetu" alisema Akson.

Mratibi wa mkesha huo Askofu Godfrey Malesi alisema hivi sasa kila Januari Mosi mikoa 17 hapa nchini imekuwa ikifanya mkesha huo ikiwepo na Zanzibar kwa ajili ya kuwaombea viongozi wa nchi na taifa kwa ujumla.

"Mungu amekuwa akijibu maombi yetu tangu tuanze kuomba kupitia mkesha huu tulipoanza jijini Dar es Salaam mwaka 1997" alisema Malesi.

Alisema tangu wakati huo wamekuwa wakiiombea nchi iwe na amani na kuondokana na ufisadi na kumpata Rais atakayeifanya Tanzania iwe mpya ambapo amepatikana Rais Dk.John Magufuli ambaye ameifanya nchi kuwa na muelekeo mpya. Alisema lengo lao ni kuhakikisha mkesha huo unafanyika katika mikoa yote na kila eneo la nchi yetu.

Mkesha huo uliopambwa na nyimbo kutoka kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam na Brass Band ya Polisi ulihudhuriwa na viongozi wa dini kutoka nchi za jirani za Rwanda na Burundi ambao walipata fursa ya kuzungumzia umuhimu wa nchi kuwa na amani.


Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson (katikati), Mratibu wa mkesha huo Askofu Godfrey Malesi na Askofu Damas Kenasi (kulia), wakishiriki kuomba katika mkesha huo.
Waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakiimba nyimbo za kumsifu mungu.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...