NA VICTOR MASANGU, MAFIA  

WAKATI serikali ya awamu ya tano ikiwa ni mpango wa kuhakiisha inajenga zahanati katika kila kijiji katika nchi nzima wananchi katika baadhi ya maeneo mengine wanakabiliwa na  changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa vifaa tiba, madawa, wauguzi, madaktari  pamoja na huduma ya upatikanaji wa mashine ya X-Ray  hali inayopelekea  wagonjwa kushindwa kupatiwa matibabu kwa wakati unaotakiwa.

Changamoto hizo zimebainika baada ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo wakati wa ziara yake ya kikazi  katika Wilaya ya Mafia iliyopo Mkoani Pwani  kwa ajili ya kuweza kukagua shughuli mbali mbali za miradi ya  kimaendeleo ikiwa pamoja na   kuweza kubaini changamoto  na matatizo yanayokakabili wananchi.

Naibu Waziri Jafo mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku moja ameweza kuzungumza na watumishi na kusema kwamba amesikitishwa sana na hali  inayowakabili wananchi wa Mafia hususan katika sekta ya afya kwani kwa sasa  wapo katika wakati mgumu kutoka na na kukosa huduma ya mashine ya X-Ray kwa kipindi cha miezi sita sasa hivyo kuwalazimu baadhi ya wagonjwa kwenda kupatiwa matibabu Jijini Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa boti au ndege.

“Kwa kweli mimi kama kiongozi wenu hili jambo la wananchi wa Wilaya ya Mafia kutokuwa na huduma ya X-Ray sio sahii kabisa hata kidogo yani wataalamu ndani ya miezi mitatu mmeshindwa kulitafutia ufumbuzi wakati wananchi wanaendelea kupata tabu na ukizingatia mtu akiumwa wakati yupo huku mafia inakuwa ni vigumu sana kumsafirisha kwenda Dar es Salaam kutibiwa, na ukizingatia gharama yenyewe ni kubwa”alisema Jafo kwa masikitiko.
Jafo alisema kwamba kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo ya ukosefu wa  huduma ya X-ray aliahidi kulishughulikia kwa hali na mali ili  kuweza kuwasaidia wananchi wa Mafia waweze kupatiwa matibabu yanayostaili na sio kupata tabu wakati serikali yao ipo kwa ajili ya kuweza kuzitatua changamoto walizonazo.

Kwa upande wake  Mganga mkuu wa Wilaya ya Mafia Joseph Mzimbe amekiri kuwepo kwa tatizo hilo la kutokuwa kwa huduma ya X-Ray na kudai kwa sasa wagonjwa wengine pindi wanapohitaji huduma hiyo wanashindwa kufanyiwa vipimo kutoka na gharama ya usafiri kutoka Mafia hadi kupelekwa katika hospitali zilizopo  Dar es Salaam ni kubwa

Naye mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Hamisi Mshilazi  akizungumza kwa niaba ya wenzake,amesema kuwa mashine hiyo ya X-ray  kwa upande ni tatizo sugu kutokana na kuharibika mara kwa mara hivyo kuzolotesha utoaji wa huduma kwa wagonjwa na kubainisha gharama ya usafiri  wa boti na ndege ni kubwa hivyo wanajikuta  baadhi yao wenye kipato cha chini wanashindwa  kwenda  kupelekwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi katika hospitali ya Taifa ya  Muhimbili.

Riziki Mngwari  yeye ni Mbunge wa viti maalumu ambaye anaiwakilisha Wilaya ya Mafia Mkoa wa Pwani kupitia  (CUF) ambaye alikuwepo katika ziara hiyo hakusita kutoka kilio chake kwa serikali ya awamu ya tano katika kuwaboreshea huduma ya afya  wananchi eneo hilo kwani wanateseka sana katika kupatiwa matibabu yanayostahili.

WANANCHI wa Wilayani ya Mafia Mkoa  Pwani  kwa sasa hawana  huduma yoyote ya mashine ya X-ray hivyo kuwalazimu baadhi ya wagonjwa kutumia gharama kubwa kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu zaidi katika hopsitali zilizipo Jijini Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa ndege au kwa boti ambayo kutokana na gharama yake kuwa ni kubwa wanashindwa kuimudu hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kutoka serikalini ili kuweza kuboresha sekta ya afya.
 Naibu Waziri ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo akiwasili katika uwanja wa ndege wa Mafia Mkoani Pwani kwa ajii ya ziara yake ya kikazi kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo na kuweza kubaini changamoto za wananchi zinazowakabili.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Seleman Jafo akisaliamina na baadhi ya viongozi na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani mara baada ya kuwasali kwa ajili ya kuendelea na ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo
Naibu Waziri akizungumza na baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Mafia wakiwemo walimu wa sekondari  hawapo pichani wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo Wilayani humo,(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...