Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe
(katikati) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji
(R) Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) alipotembelea kituo cha kupigia kura cha
Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani leo. Kulia Msimamizi
Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman Hamza.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya
Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (kulia) akiangalia Orodha ya majina ya wapiga
kura 603 iliyobandikwa katika kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi ya
Nyamanzi katika jimbo la Dimani Zanzibar leo. Kulia ni Msimamizi Msaidizi wa
Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman Hamza.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mst.
Zanzibar, Mhe. Hamid M. Hamid (katikati) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) na
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe mara baada ya
kutembelea kituo cha kupigia kura cha Dimani leo visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya
Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu wa Zanzibar, Hamid M.Hamid (wa pili kutoka kushoto) na Watendaji wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi leo mara baada ya kutembelea vituo vya kupigia kura katika jimbo la
Dimani. Katikati ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa jimbo la Dimani Bi. Idaya
Selemani Hamza, Mkurugenzi wa huduma za kisheria, Bw. Emmanuel
Kawishe (wa pili kutoka Kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Mhandisi Isack Manyiri.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...