Uongozi
wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) unatoa taarifa kuwa leo Januari 29, 2017 mnamo saa 9:40
alasiri treni ya abiria ya Deluxe ilipokuwa ikirejea Dar es Salaam kutoka
Kigoma imepata matatizo kati ya vituo vya Ruvu na Ngeta ambapo mabehewa
9 yamepata ajali. Kati ya hayo manne yameanguka, mawili yametenguka na matatu
yameacha njia.
Imeripotiwa watu kadhaa wamepata majeraha
mepesi isipokuwa mmoja ndiye aliyepata majeraha makubwa ambaye amekimbizwa
hospitali kwa matibabu zaidi.
Hizi ni taarifa za awali baada ya Kikosi cha
uokoaji kikimaliza kazi ya kuinua mabehewa ndio taarifa ya kamili ya ajali itakamilika.
Wakati taarifa hii ikipatikana Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd
Masanja Kungu Kadogosa na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Mhandisi S.
Chillery wako katika eneo la ajali.
Halikadhalika taarifa imefafanua kuwa sehemu ya
treni ya Deluxe yenye mabehewa kumi na abiria wake iko njiani kuja Dar es
Salaam na inatarajiwa kuwasili saa 2
usiku.
Aidha
uongozi wa TRL umeuhakikishia umma na
wateja wake kuwa njia ya reli kati ya Ruvu
na Dar es Salaam itafunguliwa ndani ya saa 24 ili shughuli za usafirishaji zirejee kama kawaida.
Imetolewa na Afisi ya
Uhusiano:
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Ndugu Masanja Kungu
Kadogosa
Januari 29, 2017
DAR ES SALAAM
Baadhi ya Mabehewa ya treni ya Delux ikitokea Kigoma kwenda jijini Dar
es Salaam yakiwa yameanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29,
2017.
Baadhi ya Mabewa mengine yakiwa yameacha njia
Baadhi ya Abiria waliokuwa wamepanda treni ya Delux kuokea Kigoma kuelekea jijini Dar
es Salaam wakitoka kwenye mabehewa hayo mara baada ya kupata ajali eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29,
2017.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...