Mkuu wa Wilaya ya Makete Veronica Kessy

Na Edwin Moshi, Makete
HERI YA MWAKA MPYA!
Ndugu wananchi wa Makete na Watanzania wote kwa ujumla,wananchi wa kijiji cha Isapulano katika kata ya Isapulano hapa Wilayani Makete wamepatwa na maafa mnamo tarehe 02/01/2017.
Maafa hayo yalisababishwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo,jumla ya nyumba 16 zenye jumla ya watu 37 ziliathirika kwa viwango tofauti.
Katika tukio hilo waliumia watu wawili,wakapatiwa matibabu katika Zahanati ya Isapulano na kwa bahati nzuri wanaendelea vizuri,Aidha tunamshukuru Mungu hakuna mwananchi aliyefariki.
Ndugu wananchi nyumba hizo zinahitaji vifaa vya ujenzi yaani matofali, saruji, mbao, misumari, mabati n.k, pia wananchi walioathirika wanahitaji kusaidiwa mahitaji ya kibinadamu kwa hiyo nawaomba wananchi na wadau wote wa ndani na nje ya Wilaya ya Makete tuguswe kwa namna moja ama nyingine kuchangia fedha au vitu ili kuwasaidia wananchi hao.
Kwa sasa wananchi hao wamehifadhiwa na majirani na ndugu zao,Aidha wananchi wa kijiji hicho wameanza kujitolea kusaidia ujenzi huo.
Ninawashukuru na kuwapongeza kwa jitihada hizo,nawasihi tuwaunge mkono kwa kutoa misaada ya hali na mali,michango ya fedha iingizwe kwenye Akaunti ifuatayo iliyopo NMB MAKETE.
Jina la Akaunti:Kijiji cha Isapulano
Namba ya Akaunti:60410004408
Na msaada wa vitu au vifaa uwasilishwe kwa Mtendaji wa kata ya Isapulano Bi.Tabu Mohamed mwenye namba 0745571046
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...