Na
Zuena Msuya, Mbeya
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (
PAC) imetoa miezi sita kwa Taasisi na
Mashirika yote kulipa madeni ya ankara wanayodaiwa na Shirika la Umeme nchini
(TANESCO) na endapo watashindwa kufanya hivyo watakatiwa huduma hiyo.
Agizo hilo limetolewa mkoani Mbeya na Mwenyekiti
wa Kamati ya PAC , Livingtone Lusinde wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo
wakati wa kukagua matumizi halisi ya fedha za Serikali katika kutekeleza Miradi
ya Umeme Vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati wa Vijijini( REA) kwa
kushirikiana na Shirika la Umeme nchini Tanesco.
Lusinde alisema Tanesco imekuwa ikishindwa
kutimiza majukumu yake kutokana na kukosa fedha za kutosha kujiendesha na hivyo
kuwakosesha wananchi hudumu muhimu ya umeme katika maeneo mbalimbali .
" Tanesco imetapakaa nchi nzima, lakini haiwezi
kutoa huduma bora za uhakika kwa wateja wake katika maeneo yote hayo kutokana
na miundominu mibovu na kutomfikia mteja kwa wakati kwa vile tu hawana fedha",
alisema Lusinde.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali( PAC), wakielezwa na Naibu Waziri
wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani( katikati) namna ambavyo kifaa maalum
kinachofahamika kama umeme tayari( UMETA) umeme tayari kinavyofanya kazi,
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC),
wakiwa katika ziara ya kukagua matumizi halisi ya fedha za Serikali katika
utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini.
Wafanyakazi wa Kampuni ya JV State Grid wanaotekeleza
Miradi ya Umeme Vijijini katika wakiendelea na kazi ya kujenga miundombinu ya Umeme
Vijijini katika kijiji cha Masukulu wilayani Rungwe.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC),
wakiwa katika ziara ya kukagua matumizi halisi ya fedha za Serikali katika
utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard
Kalemani(kulia), Mwenyeketi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali(
PAC) Livingstone Lusinde (katikati) wakisaini vitabu vya wageni katika Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, wakati wa ziara ya kukagua miradi ya umeme vijijni
wilayani humo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...