Rais wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu (kulia) akizungumza
wakati wa mkutano wake na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa
Sospeter Muhongo (katikati). Mkutano huo ulijadili masuala mbalimbali mojawapo
ikiwa ni uboreshaji wa Bomba la Mafuta Ghafi la TAZAMA. Kushoto ni Balozi
wa Tanzania Nchini Zambia, Balozi Grace Mujuma.
Rais wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu (kushoto)
akizungumza jambo Ikulu ya Zambia Jijini Lusaka mara baada ya kumaliza mkutano
wake na Ujumbe kutoka Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo (kushoto kwake). Kulia ni Balozi
wa Tanzania Nchini Zambia, Balozi Grace Mujuma na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Tanzania, Profesa Justin Ntalikwa.
Rais wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu (kushoto)
akifurahia jambo na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter
Muhongo mara baada ya kumalizika kwa mkutano uliofanyikia Ikulu ya Zambia.
Rais wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu (wa tatu kushoto
mstari wa nyuma) katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Tanzania na Baadhi ya
Mawaziri wa nchini Zambia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...