TAARIFA
KWA UMMA Dar es Salaam Januari 13, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti
inapenda kuwataarifu wateja wake na umma na kwa ujumla kuwa kuna video
isiyo na maadili inaiyosambazwa katika mtandao ya kijamii ikionesha
msanii akiigiza na kuimba wimbo wenye mahadhi ya taarabu mbele ya bango
lenye nembo ya bia Serengeti Premiur Lager.
Tunapenda
kuweka bayana kuwa onesho la msanii huyo halikuidhinishwa wala
kudhaminiwa na SBL Pia msanii huyo sio sehemu na hajawahi kuwa mmoja wa
mawakala wetu wanaotoa huduma za kutangaza bidhaa zetu.
Video
hiyo ambayo haizingatii maadili ya sanaa inatoa picha mbaya jambo
ambalo ni kinyume na sera ya SBL ya kuzingatia maadili mema katika
shughuli za kutangaza bidhaa zake. Aidha ikumbukwe kwamba SBL imekuwa
mstari wa mbele katika kulinda na kusimamia maadili katika shughuli zake
za kijamii ikiwa ni pamoja na kuhamasisha unywaji wa pombe kistaarabu.
Tunauhakikishia
umma na wateja wetu kuwa SBL inafanya shughuli zake za kijamii kwa
kuangalia mambo yenye tija kwa jamii na sio vinginevyo. Tunapenda
kuwashukuru sana wateja wetu na umma kwa ujumla kwa kuendelea
kushirikiana nasi.
Imetolewa na Mkurungezi wa Mahusiano
Serengeti Breweries Limited.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...