Na Stella Kalinga, Simiyu
Serikali  Mkoani  Simiyu imedhamiria kwa mwaka 2017 kutatua na kuondoa migogoro yote  ya  ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kwa wananchi wa mkoa huo.
Akitoa ufafanuzi wa namna ya  kutatua kero hiyo wakati wa mkutano wake na wananchi wa jimbo la  Meatu ,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka alisema kuwa amechoshwa kusikia na kuona migogoro ya ardhi  inayojitokeza ndani ya mkoa wake, hivyo mwaka 2017 ndio utakuwa mwisho wa kero hizo.
Mtaka amesema kuwa kamwe hawezi kukubali kuona migogoro  hiyo inaendelea hivyo wananchi na watendaji wa idara ya ardhi wanapaswa kila mmoja ajue utaratibu sahihi wa utoaji na ununuaji wa ardhi ili kuepusha sintofahamu zinazojitokeza.
“ mwaka huu  wa 2017 ni mwaka ambao mimi mkuu wa Mkoa wa Simiyu nimeamua kusimamia, kusikiliza na kutatua kero zote za ardhi… Nataka ndani ya kipindi hichi ifikie mahali migogoro ya ardhi kwa mkoa wa Simiyu inakuwa sio kipaumbele chetu… alisema Mtaka.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akiwa na Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Simiyu kupitia CCM, Mhe. Leah Komanya wakizungumza na wananchi wa Wilaya ya Meatu katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kituo cha Mabasi cha Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wilayani humo.
 Ndg. Ngodongo Maganga mkazi wa kijiji cha Cambala wilayani Meatu akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) kero yake ya kuporwa eneo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kituo cha Mabasi cha Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wilayani humo.
 Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilonga, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Meatu, Fabian Manoza, Mbunge Viti Maalum, Mhe. Leah Komanya, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini wakimkabidhi mabati Bibi Yunge Masanja yaliyotolewa na Mhe.Mbunge Komanya ili kumsaidia katika ujenzi wa nyumba yake.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Simiyu, Mhe. Leaah Komanya wakizungumza na Bibi Yunge Masanja mara baada ya kumkabidhi mabati yaliyotolewa na Mbunge huyo kwa lengo la kumsaidia kujenga nyumba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...