Na Woinde Shizza, Arusha

HALMASHAURI ya jiji la Arusha imeifungia kwa muda usiojulikana shule ya msingi Hazina Mision iliyopo kata ya Baraa, baada ya uongozi wa shule hiyo kushutumiwa kwa makosa mbali mbali ikiwemo kuwatelekeza watumishi wake pamoja na mindombinu kuwa chini ya viwango vinavyohitajika katika uandikishaji wamafunzi wa shule hiyo.

Hatua hiyo ya kufungiwa kwa shule hiyo imekuja baada ya siku chache zilizopita wamiliki wa shule hiyo kulalamikiwa kuwanyanyasa na kushindwa kuwalipa mishahara watumishi na walimu wa shule hiyo na hivyo kutakiwa kufanya marekebisho na kuwalipa stahiki watumishi lakini wakakaidi kufanya maagizo hayo kwa muda waliopewa.
Akitoa agizo hilo katika viwanja vya shule hiyo, kaimu afisa elimu shule za msingi katika jiji la Arusha, Eunice Elibariki alisema kuwa wameamua kusimamisha huduma ya utoaji elimu kutokana na shule hiyo kushindwa kufanya marekebisho waliyotakiwa kuyafanya shuleni hapo.

Alisema kuwa awali kabla hatua hiyo haijafikiwa walipata taarifa kuwa uongozi wa shule hiyo inawanyanyasa walimu kwa kuwanyima mishahara yao, kutokuwa na mindombinu kuachilia viwango pamoja na kuwepo uchafuzi wa mazingira na ndipo uongozi ukapewa muda wa kufanya marekebisho hayo pamoja na kimaliza migogoro ya kimaslahi lakini walikaidi kutoa ushirikiano hali iliyopelekea halmashauri hiyo kuchukua hatua ya kusimamisha utoaji huduma.

"Kwa kuwa uongozi wa shule hii mlishindwa kufanya marekebisho mliyoagizwa ikiwa ni pamoja na kishindwa kumaliza migogoro ya walimu kuanzia sasa nasimamisha huduma za masomo hadi hapo mtakapoweza kuiweka shule yenu katika mazingira yanayohitajika kwani lazima shule iwe na viwango na sifa zinavyohitajika sio tu kuendesha kiholela "alisema Eunice

Wananchi wa eneo hilo akiwemo Diwani wa kata ya baraa, Elifasi Ndetika akizungumzia uamuzi wa kufungiwa kwa shule hiyo alisema kuwa ni halali kabisa kwani walikuwa na malumbano ya muda mrefu baina ya uongozi na walimu lakini walishindwa kumaliza wenyewe huku akidai kuwa mazingira yalikuwa hayadhirishi na hivyo kupitia usimamishaji huo unaweza kupelekea marekebisho yakawepo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...