Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Wananchi wa Mkuranga wameibua sakata la kuibiwa kwa dawa za serikali katika hospitali yao na kutaka majibu katika mkutano wa mbunge wa jimbo la mkuranga, Abdallah Ulega.
Wananchi hao walisema wizi wa dawa za serikali unawakera kutokana kila wanapokwenda hospitali hiyo wanaambiwa wakanunue dawa huku wakitoa sh.10000 na dawa hawapati.
Akizungumza na wananchi wa Mkuranga Mbunge wa Jimbo hilo, Abdallah Ulega amesema suala la kuibiwa kwa dawa haliwezi kuvumilika kutokana na wananchi wanakwenda hospitali na kuambiwa dawa wakanunue nje.
Amesema hakuna sababu wananchi kutoa sh.10000 wakati dawa au vipimo hawapati huku na maneno yasiyostahili wakipewa.
Amesema kuna umuhimu wa fedha wanayoitoa kuungani Huduma ya Afya ya Jamii (CHF).
Ulega amesema kuwa katika ziara ya vijiji 90 licha wananchi wamekuwa wakihoji upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya na kusema wanawajibu kama baraza la madiwani kuangalia thamani fedha hiyo na huduma wanayoipata kutokana mazingira wanayoipata fedha hiyo ni magumu.
Akuzungumzia suala hilo, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Gilberto Sanga amesema mtu aliyekamatwa na dawa haitakiwi kufanyiwa uchunguzi na kumtaka Mkurugenzi wa Wilaya hiyo suala hilo kushughulikia mara moja
Mbunge wa Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa vijiji vya mkuranga katika mkutano hadhara alioutisha kwa ajili ya kupata taarifa ya maendeleo.
Mkuu wa
Wilaya ya Mkuranga Filberto Hassan Sanga akizungumza katika mkutano wa
hadhara uliotishwa na mbunge wa jimbo la Mkuranga. 03.Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mkuranga Msham Munde akizungumza katika mkutano wa vijiji
vya vya Mkuranga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga,
Juma Abeid akizungumza juhudi mbalimbali za. Halmashauri hiyo katika mkutano wa
hadhara uliotishwa na mbunge wa jimbo hilo.
Sehemu ya wananchi wa Mkuranga waliofika katika mkutano wa hadhara uliotishwa na mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega.
Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...