SERIKALI
imezitaka taasisi zake kote kuachana na mpango wa kujenga Vituo binafsi
vya vya kuhifadhia kumbukumbu (Data Center) na badala yake kutumia
Kituo cha Serikali cha kuhifadhia Data na kumbukumbu (NIDC) chenye uwezo
na hadhi ya Kimataifa. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa baada ya kufanya
ziara ya kutembelea kituo hicho cha Kimataifa cha kuhifadhia kumbukumbu
za kimtandao na Makao Makuu ya Kampuni ya Simu Tanzania TTCL.
Mheshimwa
Mbarawa amesema, Serikali imetumia fedha nyingi sana kujenga miundo
mbinu ya kituo hicho mahiri katika eneo lote la Afika Mashariki na
kusisitiza kuwa, Taasisi za Serikali ni lazima zitumie kituo hicho na
kwa zile zenye mpango wa kujenga vituo binagsi, ziachane na mpango huo
ambao ni matumizi mabaya ya fedha za Umma.
'Natoa
agizo kwa taasisi zote za Umma, ziachane kabisa na mpango wa kujenga
Data Centres. Serikali imebeba jukumu hilo, imejenga kituo cha hadhi ya
juu kabisa, sote tukitumie kituo hiki. Kila taasisi zijikite katika
majukumu yao ya msingi, hili la Data Centre watuachie Serikali kwa kuwa
tumeshalitekeleza, hatuwezi kuendelea kutumia fedha nyingine kwa eneo
hili, tuelekeze fedha hizo katika maeneo mengine muhimu.'
Akiwa
katika Makao Makuu ya Kampuni ya Simu nchini TTCL, Mhe Mbarawa ameitaka
Menejimenti ya Kampuni hiyo kuongeza kasi ya utendaji kazi na ubunifu
ili kukabiliana na ushindani uliopo katika sekta hiyo sambamba na
kukidhi kiu ya Wananchi ya kupata huduma Shirika lao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...